Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda muonekano wa giza basi habari njema ikufikie kwani hivi karibuni facebook imeongeza sehemu ya Dark mode kwenye tovuti yake ya Facebook.

1 Answer

by
+1 vote
 
Best answer

Dark Mode ni sehemu ambayo inakusaidia kupunguza mwanga mweupe kwenye programu mbalimbali ili kulinda macho yako hasa wakati wa usiku. Sehemu hii inapatikana kwenye programu mbalimbali ili kusaidia mtu yoyote kuweza kusoma vizuri hasa wakati wa usiku.

Hivi karibuni facebook imeongeza sehemu mpya ya dark mode kwenye programu yake ya kompyuta, hivi ndivyo unavyoweza kuwasha sehemu hiyo.

Tembelea tovuti ya facebook kisha kwenye sehemu ya profile yako bofya hapo na angalia mwisho kabisa utaona sehemu imeandikwa Switch to New Facebook.


Baada ya hapo utapelekwa kwenye muonekano mpya wa facebook, moja kwa moja bofya tena sehemu ya profile yako kisha angalia kwenye list hiyo na utaona sehemu mpya ya Dark Mode. Bofya hapo kuweza kuwasha.,


Baada ya hapo utaweza kupata muonekano wa giza moja kwa moja kwenye tovuti ya facebook. Kumbuka njia hii inafanyakazi kama unatumia kompyuta.

image

add
...