Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanamiliki kompyuta na ungependa kujua jinsi ya kutumia internet ya simu kwenye kompyuta basi majibu ya swali hili yako hapa.

1 Answer

by
+1 vote
 
Best answer

Siku hizi smartphone zimekuwa na uwezo wa kufanya kila kitu lakini ni kweli kwamba kuna wakati tunahitaji kompyuta ili kuweza kukamilisha baadhi ya mambo muhimu ambayo ni ngumu kufanywa kwa ustani na smartphone, kupitia hapa nitakuelekeza jinsi ya kutumia internet ya simu kwenye kompyuta.

Tethering ni nini

Tethering ni kitendo cha kutumia simu yako kama modem au ni sawa na kusema ni kitengo cha kugawana unganisho la mtandao kati ya kifaa cha rununu na kompyuta zingine zilizounganishwa.

Hotspot ni nini

Hotspot ni kitendo cha kuunda mtandao wa Wi-Fi ambapo simu hufanya kama modem / router.

Sasa ili kusudi uweze kutumia internet ya simu yako kwenye kompyuta ni muhimu kujua kuhusu ilo. Sasa kama unatumia simu ya Android hebu sasa moja kwa moja twende nikuonyeshe njia ya kutumia internet ya simu yako kwenye kompyuta.

Hatua ya kwanza chukua simu yako kisha ingia kwenye Network and Internet kisha utaona sehemu iliyo andikwa Hotspot and Tethering. Bofya hapo kuendelea.


Baada ya hapo chagua njia unayotaka kutumia, zipo njia mbalimbali kama kompyuta yako inayo WiFi basi tumia sehemu ya hotspot, kama kompyuta yako Haina sehemu ya hotspot basi moja kwa moja tumia sehemu ya USB Tethering au kama kompyuta yako inayo bluetooth unaweza kutumia Bluetooth Tethering.


Baada ya hapo washa sehemu husika kwa kubofya kitufe cha kuwasha pembeni ya njia unayotaka. Kumbuka kama umechagua hotspot ni muhimu kukumbuka kuweka password ya wifi yako.

add
...