Karibia kila siku tumekuwa tukipata maswali watu wakiuliza jinsi ya kupata simu iliyopotea, Maswali haya yamekuwa mengi sana kiasi kwamba imebidi kutoa ufafanuzi na baadhi ya njia ambazo unaweza kuzitumia kupata simu iliyopotea.

2 Answers

by
+3 votes
 
Best answer

Kwa kuanza labda nikwambie ni muhimu kuwa muangalifu pale unapo nunua simu hakikisha unahifadhi IMEI namba ya simu yako mahali ambapo unajua unaweza kuipata pale unapo hitaji. IMEI namba ni muhimu kwa sababu hii ni sawa na namba ya utambulisho ya simu yako ndio maana ni muhimu kuwa nayo pembeni.

Jinsi ya kupata simu iliyopotea kwa kutumia IMEI

Kitu cha msingi cha kufahamu zipo programu nyingi sana zinazodai kuwa zina uwezo wa kupata simu iliyopotea kwa kutumia IMEI namba, lakini programu hizi nyingi sio za kuaminika kwa asilimia 100. Pia wapo watu au makampuni ambayo hutoa huduma ya kupata simu iliyopotea lakini pia hakuna uhakika wa asilimia 100 wa kupata simu yako kwa kutumia huduma hizo.

Baadhi ya apps ambazo pia zipo Play Store kwajili ya kutoa huduma hii nyingi zinalalamikiwa kwa kutofanya kazi kwa usahihi, moja ya App hiyo unaweza kuangalia hapa.

Njia ya Kupata Simu Iliyopotea Tunayopendekeza

Hakikisha unatoa taarifa polisi kwani hapa Tanzania Sasa kuna kitengo cha cyber crime ambacho kipo karibia kwenye kila kituo cha polisi ambacho kitengo hichi ushirikiana na TCRA kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Hivyo basi hatua ya kwanza ni kutoa taarifa polisi hakikisha taarifa zako zinakuwa na IMEI namba au risiti ya simu ulipo nunua japo hii hua haitajiki sana.

Hatua ya pili wasiliana na kampuni ya kutoa huduma za simu uliyokuwa unatumia kabla ya simu yako kuibiwa, hakikisha unakuwa na IMEI ya simu yako kabla ya kutoa taarifa.

Hatua ya tatu hapa sasa ndipo jaribu kutumia programu mbalimbali za kupata simu iliyopotea kwa kutumia IMEI, hakikisha unafuata hatua zote kisha ndipo ujaribu programu hizi kwani hii itaongeza nafasi ya simu yako kupatikana.

by
+1 vote
Asante hii imenisaidia sana kweli.
add
...