Kama kwa namna yoyote simu yako imekubwa na tatizo la kutoku chaji unaweza kufuata hatua hizi chache ambazo zinaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo hilo. Kumbuka hatua hizi zinaweza kusaidia watu wote iwe una smartphone au simu ya kawaida.

1 Answer

by
+1 vote
 
Best answer

1. Badilisha Waya

Hatua ya kwanza ya kufanya ni kubadilisha waya, hii ni muhimu na ya kwanza kwa sababu wakati wote kama simu yako ilikuwa inachaji na baadae ikawa haichaji basi kuna uwezekano waya wa chaji yako umeharibika. Pia unaweza kuangalia kichwa cha chaji kama simu yako ni smartphone.

2. Subiri kwa Muda Ndipo Uchaji Tena

Kama kwa namna yoyote simu yako ilikuwa inachaji na gafla haichaji basi unaweza kujaribu kuiacha kwanza alafu ujaribu kuchaji baadae, njia hii ni nzuri sababu inakusaidia kama kuna tatizo unaweza kulijua kwanza kabla ya kulazimisha kuchaji.

3. Kama simu Imeingia Maji Iweke Kwenye Mchele Kwanza

Njia nyingine ambayo inaweza kusaidia ni pamoja na njia ya kuweka simu kwenye mchele mkavu kama imeingia maji, hakikisha unaiweka kwenye mchele alafu unaweka kwenye chombo ambacho hakipitishi hewa hii inasaidia kutoa maji yaliyopo kwenye sehemu ya kuchaji.

add
...