Je unawezaje kuhamisha majina kutoka kwenye simu yako ya zamani ya Android kwenda kwenye simu yako mpya ya iOS.?

1 Answer

by
+1 vote
 
Best answer

Jinsi ya kuhamisha majina kutoka mfumo wa Android kwenda iOS ni rahisi, zipo njia mbalimbali ambazo unaweza kutumia kuhamisha majina lakini leo nitakuonyesha njia ambayo ni rahisi zaidi.

Kwa kuanza unatakiwa kuingia kwenye soko la Play Store kisha download app inaitwa Move to iOS, unaweza kudownload app hiyo kupitia HAPA. Baada ya hapa install vizuri app hii kwenye simu yako ya Android kisha fungua app hiyo na washa Wifi (hotspot) kisha unganisha kwenye simu yako mpya ya iPhone.


Baada ya hapo anza kufanya restore na hamisha majina, picha na vitu vingine moja kwa moja.

add
...