Je unawezaje kuwasha dark mode kwenye app ya whatsapp ya Android.?

2 Answers

by
+2 votes
 
Best answer

Whatsapp dark mode ni sehemu mpya ambayo imeletwa na facebook kupitia app yake ya whatsapp, sehemu hii inakupa uwezo wa kuwasha muonekano wa giza au dark mode ambao utakuzuia usiweze kuumia macho hasa unapokuwa unatumia programu hiyo wakati wa usiku.

Jinsi ya kuwasha Dark Mode kwenye WhatsApp

  • Fungua App ya WhatsApp
  • Bofya vitufe vitatu vilivyopo juu upande wa kulia
  • Kisha chagua Settings.
  • Bofya Chats.
  • Bofya Theme alafu chagua Dark.

Kwa kufanya hivyo utaweza kupata muonekano wa Giza moja kwa moja kwenye programu ya whatsapp kupitia simu yako ya Android.

by
Kama unataka kujifunza jinsi ya kuwasha dark mode kwenye iphone unaweza kusoma hapa. Njia hii ni rahisi kama ilivyo kwenye Android.
by
0 votes
Asante sana nimeipenda sana hii
add
...