Je ni njia gani ambayo naweza kutumia kujua jina la mtu anaye nipigia simu mara kwa mara bila kupokea simu yenyewe.?

1 Answer

by
0 votes
 
Best answer

Watu wengi hudhani kuwa njia rahisi ya kujua mtu anaye kupigia simu ni kwa tumia app ya TrueCaller, japo kuwa hii ni kweli lakini unatakiwa ujue kuwa truecaller inavyofanya kazi ni sawa na ambavyo inafanya mtandao wa kijamii unavyofanyakazi.

Pale unapo pakua app ya truecaller ni lazima uweke namba yako ya simu au ni lazima ujisajili kwa kutumia Google na akaunti zingine, hii hufanya truecaller kujua jina lako kamili pamoja na kupata barua pepe yako kwajili ya uhakiki zaidi.

Sasa njia bora ya kuweza kuangali mtu anaye kupigia simu ni kwa kutumia truecaller kupitia website. Hakikisha unajisajili na akaunti ambayo haina namba ya simu kisha tumia website hiyo kujua jina la mtu anaye kupigia simu.


Weka namba kwenye sehemu ya kutafuta kisha bofya sehemu ya kutafuta tengeneza akaunti kama bado huna akaunti.

add
...