Je naweza kuongeza ulinzi kwenye simu yangu ya Android, mimi ni mtumiaji wa siku nyingi wa simu za Android hivyo kuna wakati nakuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa simu yangu tena ukizingatia simu yangu haijapata mfumo mpya wa Android.?

1 Answer

by
selected by
+1 vote
 
Best answer

Ni kweli kuwa simu nyingi za Android ambazo hazipati mfumo mpya wa Android zipo hatarini kiulinzi, hii inatokana na kukosa masasisho (update) ya muhimu ya ulinzi ambayo hutolewa na kampuni husika kwenda kwenye mfumo wa mpya wa Android kila mwaka.

Ukweli ni kuwa hakuna njia ambayo inaweza kukupa usalama kwa asilimia 100 kutokana na kuwa zipo njia mbalimbali ambazo simu yako inaweza kukosa ulinzi kwa namna moja ama nyingine, lakini yapo mambo ambayo unaweza kufanya na yanaweza kusaidia kuongeza ulinzi kwenye simu yako ya Android.

Hakikisha unatumia Programu Kutoka Play Store

Moja kati ya vitu ambavyo huwa mara nyingi vinasababisha matatizo ya ulinzi ni pamoja na tatizo la watu kupakua programu ambazo hazipatikani kwenye soko la Play Store, hii huweza kuleta virus au malware kwenye simu yako na hatimaye kufanya ulinzi wa simu yako kuwa mdogo.

Hakikisha Simu Yako Inalo toleo Jipya la Android

Japokuwa simu yako inaweza kuwa haipati mfumo mpya wa Android lakini ni vyema kuhakikisha kuwa update zote zimewekwa ikiwa pamoja na masasiho ya ulinzi (security updates) ambazo hutumwa kila mwaka na kampuni husika.

Hakikisha Programu zote kwenye Simu Yako zipo Updated

Mara nyingi wabunifu wa programu kuondoa matatizo mbalimbali ya apps zao kwa kuweka matoleo mapya ya apps zao kwenye soko la Play Store, ni vizuri kuhakikisha una update programu zako kwani huwenda moja ya programu zilikuwa zinatatizo la ulinzi ambalo linaweza kupoteza usalama wa simu yako, hivyo ni vizuri kuhakikisha una update app zako zote haraka iwezekanavyo. Mengine ya ziada unaweza kusoma hapa.


add
...