Samahan ma boss wa Tanzania tech mim nilikuwa na swal kidogo kwenu ikiwa bado sijafanya maamuz ya aina yeyote nimeona bora mnisaidie swal langu ni IPI kampuni bora ambayo naweza nunua simu yake nikaifurahia? kati ya hizi Samsung galaxy na I phones? Pia nashindwa kujua ivi mtumiaji wa simu ya iPhone anatumia mfumo gan ili kupakua nyimbo,video,na app? Naomben mnisaidie kidogo

1 Answer

by
+2 votes
 
Best answer
Ukweli ni kwamba kila mtu anapendelea simu anayoitaka kutokana na sifa anazo hitaji, lakini kutokana na kuwa wewe unaonekana bado hujajua simu unayoitaka basi naweza kukushauri hivi.

Kifupi kabisa, kama unataka simu yenye uwezo wa kufanya mambo mengi ambayo utaweza kupakua nyimbo kutoka tovuti yoyote, ambayo utaweza kuibadilisha unavyotaka basi nunua simu ya Android. Kama unataka simu isiyo na mambo mengi na ambayo unataka ifanye mambo ya msingi kama kupiga simu, kupiga picha, kuchukua video na mambo mengine ya msingi na ya kawaida basi nunua simu ya iPhone.
by
Thanks, asante sana kwa majibu haya.
add
...