Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kujua jinsi ya kutoa pesa kutoka M-Pesa Mastercard kuja kwenye akaunti yako ya M-Pesa basi hizi hapa ndio njia rahisi ambazo unaweza kufanya.

- Ingia kwenye akaunti yako ya M-Pesa (* 150 * 00 #)
- Chagua namba 4 (Lipa kwa M-Pesa)
- Chagua namba 6 (M-Pesa Mastercard)
- Chagua namba 5 (Kadi Yangu)
- Chagua namba 2 (Toa Pesa kwenye Kadi)
- Ingiaza Kiasi (Enter Amount)
- Bofya 1 kuthibitisha
Na hapo pesa zako zitatolewa kutoka kwenye M-Pesa Mastercard kuja kwenye akaunti yako ya M-Pesa. Kwa sasa njia hii inafanya kazi kwa pesa zilizowekwa kwa njia ya M-Pesa Pekee na sio vinginevyo. Kama unataka kujua jinsi ya kutengeneza M-Pesa Mastercard soma hapa.