Kama wewe ni mpenzi wa simu za samsung basi ni wazi kuwa unajua kuwa kampuni hiyo iko mbioni kuzindua simu mpya za Galaxy S10, ambazo mwaka huu inasemekana simu hizi zinakuja za aina tatu ambazo ni Galaxy S10, Galaxy S10 Plus pamoja na Galaxy S10e. Kwa asa bado hakuna taarifa nyingine zaidi kuhusu simu hiyo ya tatu ila inasemekana simu hiyo ndio itakuwa toleo la bei nafuu la simu hizo mpya za Samsung.
Kujua tetesi zaidi kuhusu simu hizi unaweza kusoma zaidi hapa, pia unaweza kujua zaidi kuhusu sifa za simu hii mpya kwa kusoma hapa. Hizi hapo chini ndio picha halisi za simu hizo mpya zinazo tarajiwa kutoka tarehe 20 mwezi february, Simu hizi zinatarajiwa kuja na ukubwa wa 1TB pamoja na RAM ya GB 12.