in

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hizi hapa hatua kwa hatua jinsi ya ku-install mfumo wa Windows kwa haraka

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Kutokana na kuwepo kwa maswali mengi yanayo uliza jinsi ya kuinstall windows leo nimekuletea hatua kwa hatua jinsi unavyoweza kuinstall Windows kwenye kompyuta yako. Natumaini hii itasaidia wengi ikiwa pamoja na wewe ambae ndio mara yako ya kwanza unajiunga nasi.

Mambo ya Muhimu ya Kuzingatia

Kabla ya kuinstall Windows kwenye kompyuta yako yapo baadhi ya mambo ya kuzingatia, mambo haya yanatofautina kulingana na hali ya kompyuta yako hivyo ni vyema kama ukisoma mambo yote yanayopatikana kwenye sehemu hii.

Jambo la kwanza – Unatakiwa kuhakikisha unakuwa na programu ya Windows kwa ajili ya kuinstall kwenye kompyuta yako. Hapa ningependa kukushauri kuwa na Flash yenye programu hiyo kuliko kuwa na CD, kwani mara nyingi CD zinakuwa ni rahisi kupata michubuko na hivyo unaweza kukwama unapokuwa una install Windows kwenye kompyuta yako.

Jambo la pili – Unatakiwa kujua kama kompyuta yako inayo Windows au Haina, hili ni muhimu kwani kuna watu unakuta tayari kompyuta zao zinayo programu ya Windows hivyo wanataka kuweka toleo jipya la Windows au kufuta lile la zamani na kuweka toleo jipya, kama unataka kufuta toleo la zamani ni vyema kufanya hivyo wakati una install windows kwani hii itakuwa ni rahisi zaidi.

Jambo la tatu – Hakikisha kama unatumia laptop basi laptop yako ina chaji kwa kiwango fulani pia kama ni muhimu jaribu kuhakikisha laptop hiyo imechomekwa kwenye chaji. Kama unatumia desktop hakikisha unakuwa na uhakika kuhusu tatizo la umeme kwani kuna wakati kukitokea tatizo la umeme basi unaweza kuharibu hatua nzima na kujikuta una anza upya.

Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Kama tayari unavyo vitu vyote sasa twende hatua kwa hatua tukajifunze jinsi ya kunstall Windows kwenye kompyuta yako.

Hatua ya Kwanza – Chomeka USB au CD iliyokuwa na Windows hakikisha kompyuta yako imezimwa (kama unatumia CD weka kwanza CD kisha zima kompyuta yako au Restart), baada ya kuchomeka washa kompyuta yako kisha bofya kitufe chenye kusema boot on chagua CD kama unatumia CD na chagua USB kama unatumia USB.

Hatua ya Pili – Baada ya kompyuta kuwaka utaona Screen ya Blue ikitaka uchague lugha ambayo ungependelea kutumia, Chagua English kisha endelea kwenye hatua inayofuata.

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hatua ya Tatu – Baada ya hapo utaona kitufe cha Install bofya hapo kuendendelea.

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hatua ya Nne – Baada ya hapo unachotakiwa kufanya ni kuweka KEY za programu ya Windows ambayo unataka kuweka kwenye kompyuta yako, kumbuka KEY hizi ni kama leseni hivyo ni muhimu kuwa nazo kabla ya kuamua kuanza process nzima.

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hatua ya Tano – Baada ya kuweka KEY na kubofya NEXT sasa ni wakati wa kukubali vigezo na masharti bofya ACCEPT iliyopo chini upande wa kulia.

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hatua ya Sita – Hatua inayofuata ni muhimu sana kwani hapa ndipo pale ambapo unaweza kuchagua kati ya kuweka Windows upya kwenye kompyuta yako au kupandisha toleo jipya la Windows. Kama unataka kuweka toleo jipya basi itakubidi kuchagua CUSTOM : na kama unataka tu kuweka toleo jipya basi chagua sehemu ya UPGRADE :

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hatua ya Saba – Unapo chagua sehemu ya CUSTOM utapelekwa kwenye ukurasa mpya ambapo unatakiwa ku-format partition unayotaka kuweka Windows, Chagua partition kisha bofya Format iliyopo chini.

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hatua ya Nane – Baada ya hapo utapelewa sasa kwenye ukurasa wa kuinstall Windows na utaona Windows imeanza kuinstall, Subiri kwa muda kisha endelea kwenye hatua zinazofuata.

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hatua ya Tisa – Baada ya kukamilika utatakiwa kuseti kompyuta yako, bofya kitufe cha USE EXPRESS SETTINGS kuseti kompyuta yako kwa haraka.

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta

Hatua ya Kumi – Baada ya hapo sasa unaweza kutengeneza akaunti yako kwa kuandika jina lako au pia kama unataka kuweka password unaweza kufanya kwenye hatua hii.

Kama kuna mahali ambapo utakuwa umekwama unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Kama unataka mfumo wa Windows 10 unaweza kupakua mfumo huu mzima kupitia link hapo chini.

Download Windows 10 Hapa

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuinstall mfumo wa Windows kwenye simu yako ya mkononi ya Android.

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuinstall Windows Kwenye Kompyuta
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kufufua Spika ya Simu Yako Bila Kufungua

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments