in

Kompyuta Mpya ya Asus ROG GT51CA Kwaajili ya Game

Kompyuta Mpya ya Asus ROG GT51CA Kwaajili ya Game

Kwa wale wapenda game hivi karibuni Asus imezindua kompyuta yake ya kisasa ya Asus Rog gt51ca ambayo ni maalumu kwa game, kompyuta hiyo inakuja imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana ambapo inakuja na saa maalumu ya kuvaa mkononi ambayo inatumia (NFC) Near-Field Communication.

Kwa kutumia kifaa hicho maalumu mtumiaji wa kompyuta hiyo ya Asus Gog GT51CA anaweza kuwasha kompyuta hiyo kwa kugusa tu saa hiyo akiwa karibu na kompyuta hiyo, pia mtumiaji anaweza kuwasha sehemu maalumu ya kuhifadhi data iliyofichwa kwenye kompyuta hiyo hayo yote yanafanyika moja kwa moja kwa kutumia saa hiyo maalumu.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa upande wa sifa kompyuta hiyo inauwezo wa processor ya Intel Core i7-6700K Skylake processor ambayo ina nguvu ya 4.6GHz, pia kama ungependa kuongeza memory na graphics ya kompyuta hiyo unaweza ukaongeza mpaka GeForce GTX Titan X graphics cards pamoja na RAM mpaka GB 12 kila upande. Kwa kawaida kompyuta hiyo inayo RAM ya GB 16 ya aina ya DDR4 2133MHz memory, 2800MHz pia hard disk ya M.2 PCIe 512GB SSDs.

Kompyuta Mpya ya Asus ROG GT51CA Kwaajili ya Game
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.