in

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)

Zifahamu hapa simu hizo pamoja na bei zake pamoja na mahali pakununua

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)

Linapo kuja swala zima la kununua simu bora ni wazi kuwa kila mtu hapa anahitaji ushauri, ili kuweza kupata simu bora ya kununua tena hasa mwaka huu 2019 ambapo simu zimetoka za aina mbalimbali. Kwa kuzingatia hilo leo tumekuletea list ya simu 10 bora za kununua kwa sasa pamoja na bei zake ikiwa na mahali pa kununua simu hizi kama zinapatikana.

Basi bila kupoteza muda twende tukangalie list hii moja kwa moja, kumbuka list hii imepangwa kwa kuangalia moani mbalimbali ya watu kupitia mitandao mbalimbali.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Infinix Hot S3 X573

Infinix Hot S3 X573 ni simu bora lakini pamoja na ubora simu hii inakuja ikiwa na teknolojia mpya ya kioo cha aspect ratio ya 18:9, simu hii inakuja na muonekana mzuri na inakuja na sifa nyingine za

Sifa za Infinix Hot S3

  • OS: Android 8.0 Nougat with XOS v3.0
  • SIM Type: Dual SIM (Nano)
  • 4G LTE: YES, LTE
  • Screen Size : 5.65 Inches HD IPS Touchscreen
  • Screen Resolution: 720 x 1440 pixels (~285 PPI)
  • Processor Type: Octa-core 1.40 GHz, Snapdragon 430 chipset
  • RAM: 3GB
  • Internal Storage: 32GB
  • External Storage: microSD, up to 128GB
  • Back / Rear Camera: 13MP camera & LED Flash
  • Front Camera: 20MP with LED flash
  • Battery: 4000 mAh (non-removable)

BEI – Tsh 552,000

Tecno Camon CM

Tecno Camon CM ni simu ambayo ni bora sana kuwa nayo kwa wale wapenzi wa simu za tecno na kwa wale wanaopenda kuwa na simu zinazo zingatia bajeti ya pesa yako. Tecno Camon CM inauwezo mzuri wa kamera ikiwa na sifa nyingine kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Camon CM 2018

  • Aina ya Kioo  – Full Vision capacitive touchscreen
  • Ukubwa wa Kioo – 5.65-inch yenye resolution ya 720 x 1440 pixels
  • Uwezo wa SIM – Line mbili ndogo
  • Uwezo wa Network – 2G/3G/4G
  • Uzito wa Simu – 144g
  • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye FF pamoja na Ring-Flash (Quad-Flash)
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 13 yenye FF, pamoja na Dual-Flash
  • Uwezo wa Processor – Quad-Core 1.3GHz yenye uwezo wa 64-bit MEDIATEK MTK6737H
  • Uwezo wa GPU – Mali-T720
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 inayoweza kuongezeka kwa memory card hadi 128GB
  • Ukubwa wa RAM – GB2
  • Uwezo wa Sensors – inayo sensor za G-Sensor, Fingerprint, Ambient Light Sensor, Proximity Sensor and E-Compass
  • Mfumo wa uendeshaji – Android 7.0 Nougat yenye HiOS 2.0 User Interface
  • Uwezo wa Bluetooth – V4.1
  • Uwezo wa Battery – battery ya Li-Polymer yenye ukubwa wa 3050mAh, pamoja na teknolojia ya Fast Charging.
  • Mengineyo – Inayo fingerprint, inayo radio, kava lake ni la chuma.

BEI – Tsh 339,000

Tecno Camon X Pro

Hivi karibuni Tecno imezindua simu hii yenye sifa nzuri na muonekano bora, mbali ya kuwa na sifa na muonekano bora simu hii imeboreshwa zaidi kwenye upande wa kamera na sasa utaweza kupiga picha nzuri zaidi za Selfie, Simu hii inakuja na sifa zingine kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Camon X na X Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.00 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~269 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0GHz MediaTek Helio P23
  • Uwezo wa GPU – Mali-T720
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 kwa Tecno Camon X na GB 64 kwa Tecno Camon X Pro zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3 kwa Tecno Camon X na GB 4 kwa Tecno Camon X Pro
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 kwa Tecno Camon X Pro na Megapixel 20 kwa Tecno Camon X zote zikiwa na Ring flash
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 ikiwa na Dual-flash
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3750 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
    pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0
  • Rangi – Inakuja kwa rangi ya Midnight Black
  • Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM
  • Ulinzi – Fingerprint (iko nyuma), Face Unlock (kufungua simu kwa uso)
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G

BEI – Tsh 400,000 hadi Tsh 550,000

Tecno Phantom 8

Tecno Phantom 8 ni moja kati ya simu nzuri kutoka kampuni ya Tecno, simu hii ya mwaka 2017 ni moja ya simu ambazo bado zinadumu na bado ni simu nzuri sana. Simu hii inakuja na kamera mbili kwa nyuma pamoja na sifa nyingine kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Phantom 8

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.7 huku ikiwa na resolution ya 1920 x 1080, pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat with HiOS 3.0.
  • Uwezo wa Processor – Octa core 2.6 GHz huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya MediaTek Helio P25.
  • Uwezo wa RAM – GB 6.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G.
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 20, Huku ikiwa na Dual-LED flash.
  • Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine yenye Megapixel 13 zote zikiwa na teknolojia ya Telephoto for 2x zoom.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint iliyoko kwa nyuma.
  • Uwezo wa Battery – 3500 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion

BEI – Tsh 820,000

Nokia 6

Nokia 6 ni moja kati ya simu ambazo ni simu nzuri zinazo tambulisha ujio mpya wa kampuni ya Nokia, simu hii inakuja na maboresho mapya pamoja na sifa nzuri zenye kufanya uipende simu ya Nokia kwa mara nyingine tena. Simu inakuja na sifa nzuri kama zifuatazo.

Sifa za Nokia 6

  • Dimensions: 148.8 x 75.8 x 8.15mm
  • OS: Android 8
  • Screen size: 5.5 inches
  • Resolution: 1920 x 1080
  • CPU: Snapdragon 630
  • RAM: 3GB/4GB
  • Storage: 32GB/64GB
  • Battery: 3,000mAh
  • Rear camera: 16MP
  • Front camera: 8MP

BEI – Tsh 500,000

Apple iPhone 8

iPhone 8 ni moja kati ya simu mpya za Apple na ni simu ambayo ni bora sana kuwa nayo kwa muda huu, simu hii inakuja na sifa mpya na maboresho zaidi. Mbali na hayo simu hii inakuja na kamera nzuri sana na ni moja kati ya simu inayopendwa zaidi. Simu hii inakuja na sifa zingine kama zifuatazo

Sifa za iPhone 8

  • Ukubwa wa Simu  – 138.4mm x 67.3 x 7.3 mm
  • Uzito wa Simu – Weight: 148g
  • Ukubwa wa Kioo – Inch 4.7 yenye teknolojia ya LCD display na resolution ya 1334 x 750 / 326 ppi and 625 cd/m2 max brightness  (Retina HD display)
  • Uwezo wa Processor – six-core A11 Bionic chip with 64-bit architecture, neural engine, and M11 motion coprocessor
  • Ukubwa wa RAM – GB 2 (haijadhibitishwa)
  • Ukubwa wa Ndani – Zipo Aina Mbili GB 64 na GB 256
  • Kamera ya Nyuma – Ipo moja yenye uwezo wa Megapixel 12 yenye iSight camera with f/1.8 aperture, optical image stabilization, six-element lens
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye FaceTime camera with f/2.2 aperture
  • Ulinzi – Touch ID fingerprint sensor
  • Uwezo wa Wi-Fi – 802.11a/b/g/n/ac Wi‑Fi with MIMO
  • Uwezo wa Mtandao – LTE Advanced
  • Uwezo wa Bluetooth – Inatumia teknolojia ya Bluetooth 5.0
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 11
  • Uwezo wa Kuzuia Kuinga Maji – IP67 splash, water, and dust resistance
  • Uwezo wa Battery – Inakaa hadi masaa 14 (ukiwa unaongea), Masaa 12 (ukiwa unatumia Internet), Masaaa 13 (ukiwa unangalia video) pamoja na Masaa 40 (ukiwa unasikiliza mziki)
  • Uwezo wa Chaji – inauwezo wa fast-charging inaweza kujaa chaji asilimia 50 ndani ya dakika 30.
  • Uwezo wa Kuchaji Bila Waya – Inauwezo wa Kuchaji bila waya huku ikiwa na teknolojia ya Qi wireless charging support

BEI – Tsh 3,000,000

Samsung Galaxy S9

Hapa sidhani kama nina haja ya kusema maneno mengi, ni wazi kuwa umesha sikia matangazo mengi sana ya simu hii, mbali na simu hii kuwa na umbo na sura nzuri simu hii inakuja na uwezo mzuri sana wa kamera na hayo yakiwa ndio maboresho makubwa kwenye simu hii. Simu hii pia inakuja na sifa nyingine kama zifuatazo

Sifa za Samsung Galaxy S9

  • Mfumo wa Uendeshaji –  Android 8 (Oreo)
  • Ukubwa wa Kioo – 5.8-inch Quad HD + Curved Super AMOLED, 18.5:9 (529ppi)
  • Ukubwa wa Simu – Body: 147.7mm x 68.7mm x 8.5mm, 163g, IP68
  • Ukubwa wa Kamera – Kamera ya Nyuma Super Speed Dual Pixel 12MP AF sensor with OIS (F1.5/F2.4) Kamera ya Mbele 8MP AF (F1.7)
  • Ukubwa wa Processor – 10nm, 64-bit, Octa-core processor (2.8 GHz Quad + 1.7 GHz Quad)
  • Ukubwa wa RAM – 4GB RAM /
  • Ukubwa wa Ndani – 64GB + Micro SD Slot (up to 400 GB)
  • Ukubwa wa Battery – 3,000mAh yenye teknolojia ya Fast Wired Charging compatible with QC 2.0 / Fast Wireless Charging compatible with WPC and PMA
  • Uwezo wa Network – Enhanced 4X4 MIMO / CA, LAA, LTE Cat.18
  • Aina za Viunganishi –  Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac (2.4/5GHz), VHT80 MU-MIMO, 1024QAM, Bluetooth® v 5.0 (LE up to 2Mbps), ANT+, USB type-C, NFC, Location (GPS, Galileo, Glonass, BeiDou)
  • Aina za Sensors – Iris sensor, Pressure sensor, Accelerometer, Barometer, Fingerprint sensor, Gyro sensor, Geomagnetic sensor, Hall sensor, HR sensor, Proximity sensor, RGB Light sensor
  • Aina ya Ulinzi – Authentication: Lock type: pattern, PIN, password, Biometric lock type: iris scanner, fingerprint scanner, face recognition, Intelligent Scan – biometric authentication with iris scanning and facial recognition
  • Mengine – Virtual Reality – Gear VR with Controller (SM-R325NZVAXAR), Google Daydream View

BEI – Tsh 2,500,000

Apple iPhone 8 Plus

Kwenye namba tatu ni simu mpya ya Apple iPhone 8 Plus, hii ni simu nyingine kutoka Apple simu hii ni bora kuwa nayo kwa sasa kwa sababu simu hii inakuja na kioo kikubwa kuliko ile ya iPhone 8  ya kawaida na vilevile simu hii inakuja na ukubwa zaidi pamoja na sifa nyingine kama zifuatazo.

Sifa za iPhone 8 Plus

  • Ukubwa wa Simu  – 158.4mm x 78.1 x 7.5 mm
  • Uzito wa Simu – Weight: 188g
  • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 yenye teknolojia ya LCD display na resolution ya 1334 x 750 / 440 ppi and 625 cd/m2 max brightness  (Retina HD display)
  • Uwezo wa Processor – six-core A11 Bionic chip with 64-bit architecture, neural engine, and M11 motion coprocessor
  • Ukubwa wa RAM – GB 3 (haijadhibitishwa)
  • Ukubwa wa Ndani – Zipo Aina Mbili GB 64 na GB 256
  • Kamera za Nyuma – Zipo mbili zenye uwezo wa megapixel 12 wide-angle camera yenye f/1.8 aperture na nyingine yenye Megapixel 12 f/1.8 camera yenye f/2.8 aperture, optical zoom up to 2x, optical image stabilizatio
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye FaceTime camera with f/2.2 aperture
  • Ulinzi – Touch ID fingerprint sensor
  • Uwezo wa Wi-Fi – 802.11a/b/g/n/ac Wi‑Fi with MIMO
  • Uwezo wa Mtandao – LTE Advanced
  • Uwezo wa Bluetooth – Inatumia teknolojia ya Bluetooth 5.0
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 11
  • Uwezo wa Kuzuia Kuinga Maji – IP67 splash, water, and dust resistance
  • Uwezo wa Battery – Inakaa hadi masaa 14 (ukiwa unaongea), Masaa 12 (ukiwa unatumia Internet), Masaaa 13 (ukiwa unangalia video) pamoja na Masaa 40 (ukiwa unasikiliza mziki)
  • Uwezo wa Chaji – inauwezo wa fast-charging inaweza kujaa chaji asilimia 50 ndani ya dakika 30.
  • Uwezo wa Kuchaji Bila Waya – Inauwezo wa Kuchaji bila waya huku ikiwa na teknolojia ya Qi wireless charging support

BEI – Tsh 3,050,000

Apple iPhone X

Apple iPhone X ni moja kati ya simu za kisasa na bora sana kuwa nazo, Vilevile iPhone X ni moja kati ya simu zilizo tangulia kwenye teknolojia nadhani kuliko simu nyingine kwenye list hii, iPhone X inakuja na kioo cha kisasa cha Full Display na inakuja na uwezo wa tofauti sana pamoja na sifa zifuatazo.

Sifa za iPhone X au iPhone 10

  • Ukubwa wa Simu – 143.6mm x 70.9 x 7.7 mm
  • Uzito wa Simu – 174g
  • Ukubwa wa Kioo – inch 5.8 yenye teknolojia ya OLED True Tone display pamoja na resolution ya 2436 x 1125 resolution at 458 ppi, 625cd/m2 brightness, and 1,000,000:1 contrast ratio (Super Retina display)
  • Uwezo wa Processor – six-core A11 Bionic chip with 64-bit architecture, neural engine, and M11 motion coprocessor
  • Ukubwa wa RAM – GB 3
  • Ukubwa wa Ndani – Zipo Aina Mbili GB 64 na GB 256
  • Kamera za Nyuma – Zipo mbili zenye uwezo wa megapixel 12 wide-angle camera yenye f/1.8 aperture na nyingine yenye Megapixel 12 f/1.8 camera yenye f/2.8 aperture, optical zoom up to 2x, optical image stabilizatio
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye FaceTime camera with f/2.2 aperture
  • Ulinzi – TrueDepth camera for Face ID 3D facial recognition
  • Uwezo wa Wi-Fi – 802.11a/b/g/n/ac Wi‑Fi with MIMO
  • Uwezo wa Mtandao – LTE Advanced
  • Uwezo wa Bluetooth – Inatumia teknolojia ya Bluetooth 5.0
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 11
  • Uwezo wa Kuzuia Kuinga Maji – IP67 splash, water, and dust resistance
  • Uwezo wa Battery – Inakaa hadi masaa 14 (ukiwa unaongea), Masaa 12 (ukiwa unatumia Internet), Masaaa 13 (ukiwa unangalia video) pamoja na Masaa 40 (ukiwa unasikiliza mziki)
  • Uwezo wa Chaji – inauwezo wa fast-charging inaweza kujaa chaji asilimia 50 ndani ya dakika 30.
  • Uwezo wa Kuchaji Bila Waya – Inauwezo wa Kuchaji bila waya huku ikiwa na teknolojia ya Qi wireless charging support

BEI – Tsh 3,400,000

iPhone XS na iPhone XS Max

iPhone XS na XS Max

Kama wewe ni mpenzi wa simu za iPhone basi ni wazi kuwa iPhone XS na XS Max ni moja kati ya simu bora hasi sasa kutoka kampuni ya Apple, mbali ya simu hizi kuwa bora simu hizi ndio simu mpya kwa sasa kutoka Apple hivyo tegemea kupata kila kitu ambacho ulikuwa unakitaka kwenye simu hizi za iPhone. Simu hizi ni moja kati ya simu zenye vioo vizuri na iPhone XS Max ni toleo lenye kioo kikubwa kuliko simu zote za iPhone ambazo zimewahi kuingia sokoni.

Sifa za iPhone XS

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1125 x 2436 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~458 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12
  • Uwezo wa Processor – Hexa-core.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12 Bionic Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 256, na nyingine GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@60fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 28mm, 1.4µm, OIS, PDAF , na kamera nyingine pia inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm, 1µm, AF, OIS, 2x optical zoom.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion (ukubwa wa battery haujajulikana) battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Space Gray na Silver, Gold
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof (maji ya urefu wa 2m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).

BEI – Tsh 3,000,000 – 2,800,000

Samsung Galaxy S9 Plus

Samsung Galaxy S9 Plus ni moja kati ya simu bora sana kuwa nazo na naweza kusema kama unataka simu bora ya kuwa nayo kwa sasa unaweza kununua simu hii, simu hii ni bora sana kwa upande wa sifa pamoja na upande wa kamera, mbali na hayo simu hii ni nzuri sana kwa sura na inakuja na sifa nyingine kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy S9 Plus

  • Mfumo wa Uendeshaji –  Android 8 (Oreo)
  • Ukubwa wa Kioo –  6.2-inch Quad HD + Curved Super AMOLED, 18.5:9 (570ppi)
  • Ukubwa wa Simu – 158.1mm x 73.8mm x 8.5mm, 189g, IP68
  • Ukubwa wa Kamera – Kamera za nyuma ziko mbili Dual OIS / Wide-angle: Super Speed Dual Pixel 12MP AF sensor (F1.5/F2.4) na nyingine Telephoto: 12MP AF sensor (F2.4) kamera ya mbele 8MP AF (F1.7)
  • Ukubwa wa Processor – 10nm, 64-bit, Octa-core processor (2.8 GHz Quad + 1.7 GHz Quad)
  • Ukubwa wa RAM –  6GB RAM
  • Ukubwa wa Ndani – 64GB + Micro SD Slot (up to 400 GB)
  • Ukubwa wa Battery – 3,500mAh yenye teknolojia ya Fast Wired Charging compatible with QC 2.0 / Fast Wireless Charging compatible with WPC and PMA
  • Uwezo wa Network – Enhanced 4X4 MIMO / CA, LAA, LTE Cat.18
  • Aina za Viunganishi –  Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac (2.4/5GHz), VHT80 MU-MIMO, 1024QAM, Bluetooth® v 5.0 (LE up to 2Mbps), ANT+, USB type-C, NFC, Location (GPS, Galileo, Glonass, BeiDou)
  • Aina za Sensors – Iris sensor, Pressure sensor, Accelerometer, Barometer, Fingerprint sensor, Gyro sensor, Geomagnetic sensor, Hall sensor, HR sensor, Proximity sensor, RGB Light sensor
  • Aina ya Ulinzi – Authentication: Lock type: pattern, PIN, password, Biometric lock type: iris scanner, fingerprint scanner, face recognition, Intelligent Scan: biometric authentication with iris scanning and facial recognition
  • Mengineyo – Virtual Reality: Gear VR with Controller (SM-R325NZVAXAR), Google Daydream View

BEI – Tsh 2,315,000

Updated (Imeongezwa)  25-08-2018

Samsung Galaxy Note 9

Simu nyingine ambayo ni nzuri kuwa nayo kwa sasa ni Galaxy Note 9, mbali ya kuwa ni simu mpya kutoka kampuni ya Samsung, lakini pia ni moja kati ya simu bora sana kwa sasa. Simu hii inakuja na kioo kikubwa pamoja na uwezo mkubwa sana kama vile ukubwa wa ndani wa GB 512 pamoja na uwezo mkubwa sana wa kuweza kuimili kucheza game kwenye simu hiyo kwa muda mrefu bila simu hiyo kupata moto. Mbali ya hayo simu hii ni ngumu sana kutokana na kutengenezwa na Glass ya Gorilla Glass 6 ambayo hii ndio teknoloji mpya ya Glass ngumu za simu kwa sasa, kama uniamini unaweza kutazama video hapa.

Sifa za Samsung Galaxy Note 9

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 2960 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~514 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.7 GHz Mongoose M3 & 4×1.8 GHz Cortex-A55) – EMEA au Octa-core (4×2.7 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9810 Octa – EMEA au Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP18 – EMEA au Adreno 630.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 128, nyingine GB 512 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ina RAM ya GB 8 na nyingine ina RAM ya GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/1.7, 25mm, 1/3.6″, 1.22µm, AF yenye uwezo wa kuchukua video za 1440p@30fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.5-2.4, 26mm, 1/2.55″, 1.4µm, dual pixel PDAF, OIS na kamera nyingine pia inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm, 1/3.6″, 1µm, AF, OIS, 2x optical zoom.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (Quick Charge 2.0).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO. USB ya Type-C 3.1 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Metallic copper, Lavender purple, Ocean blue na Midnight black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof (maji ya urefu wa 1.5m kwa dakika 30), pia Inakuja na Samsung DeX kwaajili ya kutumia simu yako kwenye kompyuta.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Iris scanner, fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer, heart rate, SpO2
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Iris Scanner).

BEI – Tsh 2,900,000 – Tsh 3,000,000

Huawei P20 na P20 Pro

Sifa za Huawei P20 Pro na Huawei P20

Huawei P20 na P20 Pro ni moja kati ya simu bora sana kutoka kampuni ya Huawei, mbali ya kuwa simu bora simu hizi zinauwezo mkubwa sana wa kamera hivyo kama umekuwa ukitafuta simu yenye uwezo mzuri wa kupiga picha vizuri basi Huawei P20 na P20 Pro ni simu nzuri sana kwaajili yako. Simu hizi kwa sasa zipo hapa nchini Tanzania hivyo unaweza kuzipata kwenye maduka mbalimbali yanayo uza simu za Huawei.

Sifa za Huawei P20

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1080 x 2244 pixels, 18.5:9 ratio (~432 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 & 4×1.8 GHz Cortex-A53)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko kwa machaguo mawili GB 128 pamoja na GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko kwa machaguo mawili GB 6 na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye (f/2.0, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye (f/1.6, 1/2.3″, 1.55 µm,, OIS) na Kamera nyingine inayo Megapixel 20 yenye (f/1.6, 27mm) pamoja na teknolojia za Leica optics, 2x lossless zoom, phase detection, laser autofocus pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 3400 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue na Twilighte
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint kwa mbele

BEI – Tsh 900,000 – Tsh 1,500,000

TECNO Camon 11 Pro

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)

TECNO camon 11 Pro ni simu bora sana ya TECNO toka TECNO Phantom 8, simu hii inakuja na sifa nzuri na pia ni moja kati ya simu chache za TECNO zenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu. Simu hii mbali ya kuwa na sifa nzuri pia ni moja kati ya simu ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya TECNo kuja na ukingo wa juu maarufu kama Notch, pamoja na teknolojia ya AI kwenye kamera zake. Kama wewe ni mpenzi wa simu za TECNO na ungependa kwenda na wakati basi TECNO Camon 11 Pro ndio simu ambayo ningependa kushauri ununue.

Sifa za TECNO Camon 11 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~269 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) na HiOS 4.1
  • Uwezo wa Processor – Octa-Core 2.0GHz.
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek Helio P22 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G71 MP2.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye teknolojia ya AI pamoja na LED Flash
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine inakuja na Megapixel 5 zenye AI, Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3750 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Blue
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, Compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor na Fingerprint.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID).

BEI – Tsh 700,000 – Tsh 650,000

TECNO Pop 2F

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)

TECNO Pop 2F ni toleo jipya la simu za bei nafuu za TECNO Pop 2 ambazo zilizinduliwa rasmi mwaka 2018, simu hii inakuja na maboresho kama vile ukubwa wa ndani wa GB 16 tofauti na toleo lililopita ambalo lilikuwa na ukubwa wa ndani wa GB 8. Simu hizi ni kwa sasa zinapatikana kwa bei nafuu sana hapa Tanzania na unaweza kuzipata kwenye maduka mbalimbali hapa Tanzania.

Bei – Tsh 150,000 hadi Tsh 180,000

Soma Zaidi >

TECNO Pouvoir 3

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)

TECNO Pouvoir 3 ni simu nyingine kutoka kampuni ya Tecno iliyozinduliwa mwaka 2019, kama unavyojua kuhusu simu hizi kutoka Tecno huwa na uwezo mkubwa sana wa kudumu na chaji. Pamoja na sifa nyingine za simu hii nadhani utafurahia zaidi simu hii kwa upande wa chaji pamoja na ugumu na ubora wa simu hii.

Bei – Tsh 350,000 hadi Tsh 400,000

Soma Zaidi > 

TECNO Phantom 9

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)

TECNO Phantom 9, simu hii ni simu yenye sifa bora kuliko simu zote za tecno kwa mwaka huu 2019, mbali na hayo simu hii ni moja ya simu zilizo shikilia rekodi ya kuwa simu za kwanza za kutoka TECNO kuwa na kamera zaidi ya mbili kwa nyuma, pamoja na teknolojia mpya ya kioo cha AMOLED ambacho hakijawahi kutumiwa kwenye simu za TECNO. Unaweza kusoma hapa kujua mambo ambayo ulikuwa huyajui kuhusu simu hii. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika.

Bei – Tsh 600,000 hadi Tsh 700,000

Soma Zaidi >

TECNO Camon 12

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)

Camon 12 ni simu nyingine bora ya TECNO iliyozinduliwa mwaka 2019, simu hii inakuja na sifa bora pamoja na muonekano wa kisasa kuliko simu zote za Camon zilizotoka hadi sasa. Simu hizi zinakuja kwa matoleo matatu ya Camon 12, Camon 12 Pro, pamoja na Camon 12 Air zote zikiwa na muonekano unaofanana. Kumbuka bei inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo ulilopo.

Bei – Tsh 300,000 hadi Tsh 450,000

Soma Zaidi >

TECNO Spark 4

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)

Kampuni ya TECNO imefunga mwaka huu 2019 kwa kuzindua simu mpya ya TECNO Spark 4, simu hii ni toleo la maboresho la simu ya TECNO Spark 3 ambayo ilitoka mwaka 2018, simu hii kama ilivyo Camon 12 nayo inakuja na sifa bora pamoja na muonekano bora. Mbali na hayo simu hii nayo inakuja na matoleo mawili tofauti kama ya Spark 4 na Spark 4 Air, simu zote zinafanana kwa muonekano. Kumbuka bei inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo ulilopo.

Bei – Tsh 280,000 hadi Tsh 350,000

Soma Zaidi > 

Na hizo ndio simu bora ambazo unaweza kuzipata sasa hapa Tanzania, kumbuka bado ziko simu nyingi sana zenye uwezo mzuri sana na bado zipo simu nyingi sana zenye sifa nzuri zaidi ya hizi zilizopo kwenye list hii.  Hivyo basi, baada ya kusema hayo nini maoni yako..? tuambie unahisi kuna simu gani nzuri ambayo inapatikana hapa Tanzania ambayo inastahili kuwepo kwenye list hii tuambie kwenye maoni hapo chini. Pia kumbuka kama wewe ni mpenzi wa simu za Tecno, unaweza kusoma hapa list ya simu nzuri za tecno za kununua mwaka huu 2020.

Simu 10 Bora za Kununua Kwa Sasa na Bei Zake (2020)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

31 Comments